
Mchezaji wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Ronaldinho Gaucho hatimaye baada ya muda mrefu amerejea klabuni hapo lakini safari akifanya kazi nyingine kabisa na si kama mchezaji.
Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 36, amerudi klabuni hapo kuwa kama balozi wa klabu hiyo duniani.
Barcelona wanafungua ofisi mpya jijini New York, nchini Marekani Septemba 10 mwaka huu ili kuzidi kupanua mahushiano yake zaidi, hali iliyowasukuma kumrejesha Ronaldinho ili afanye kazi hiyo.
0 comments:
Post a Comment