MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amemzawadia gari aina ya Toyota beki wa kushoto Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kutokana kiwango kizuri anachokionesha uwanjani kwa sasa hali inayopelekea timu kupata matokeo mazuri.
Hans Poppe amesisitiza kuwa haijaishia hapo tu bali mchezaji yeyote atakayefanya vizuri zaidi kwenye klabu hiyo anaweza kulamba zawadi kama hiyo au zaidi
Hans Poppe, ambaye ni miongoni mwa watu wenye ushawishi mkubwa zaidi klabu hapo amesema zawadi hiyo ambayo imeambatana na kiasi taslimu cha sh. Milioni 1 ya mafuta kwa miezi sita, haimo kwenye vipengele vya Mkataba wake wa sasa unaomalizika mwishoni mwa msimu.
0 comments:
Post a Comment