Thursday, September 8, 2016

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Sunday Manara amesema kwamba, ushindi waliopata jana dhidi ya Ruvu Shooting ni ishara ya kuwa sasa kile walichowaahidi Wanasimba ndicho wanachokifanya uwanjani.

Kauli hiyo ya Manara imekuja mara baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa 2-1 hapo jana dhidi ya Wanajeshi hao ambao hapo awali kupitia msemaji wao waliahidi kuwafukuza kwa bakora.

Manara aliongeza kuwa, Simba ni timu kubwa na kuwapongeza wale wote waliokuwa wakipiga kelele kabla ya mchezo wa jana na kuongeza kuwa kilichowapata ndicho walichostahili.

"Nashukuru Mwenyezimungu, nashukuru fans wetu na nawapongeza waliopiga kelele kabla ya mchezo maana ndiyo sehemu ya mchezo, ajue (Masau Bwire) tu Simba ni kubwa, alisema atatufukuza na bakora, Simba ni mkali sana, tumemtafuna kimya kimya," Manara alisema.

Kuhusu safu yao ya ushambuliaji kutengeneza nafasi nyingi za magoli lakini wakishindwa kuzitumia, Manara alisema anaamini kocha wao Joseph Marius Omog atayafanyia kazi na kufanya vizuri katika michezo zijazo. 

"Mimi naamini mwalimu atayafanyia kazi mapungufu, ilikuwa tuwafunge zaidi ya magoli matano na umeona tumekosa magoli mengi sana, nadhani walimu watafanyia kazi suala la scoring (ufungaji) , timu imekosa magoli mengi sana lakini tunamshukuru Mwenyezimungu pointi tatu muhimu," aliongeza.

Simba itakuwa na kibarua kizito tena Jumapili Septemba 11 pale watakavaana na Wakata Miwa wa Manungu Turiani Morogro Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video