Bosi wa Manchester City Guardiola ameelezea heshima yake juu ya Zlatan Ibrahimovic na kusema kuwa ni moja ya wachezaji bora kabisa duniani licha ya kutokuwa katika maelewano mazuri wakati wakiwa Barcelona.
Guardiola alimpeleka Ibrahimovic kwa mkopo AC Milan baada ya wawili hao kushindwa kuelewana mwaka ambao Guardiola aliipa Barca makombe matatu (2009-10).
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa zamani wa Sweden (34), amekuwa akionesha chuki za wazi kutoka moyoni dhidi ya Guardiola na kumuita muoga na asiyejiamini.
Kuelekea mchezo huo wa Manchester derby, wakala mbwatukaji wa Ibrahimovic Mino Raiola amemtuhumu Guardiola kwa kusema ni kocha anayefundisha soka lisilovutia, lakini Guardiola amemsifu straika huyo wakati akiongea na wanahabari.
"Nina heshima kubwa sana kwa kile ambacho Zlatan amefanya katika soka," amesema.
"Ni moja ya washambuliaji bora sana na bila shaka wachezaji bora huleta matokeo ya moja kwa moja pale wanapowasili kwenye timu.
"Baadhi ya wachezaji husubiri mpaka waizoee ligi husika, lakini wachezaji bora hufanya hivyo mapema sana."
0 comments:
Post a Comment