Monday, September 12, 2016

Mbwana Samatta akicheza dakika 90 wakati klabu yake ya Genk ilipokipiga ugenini dhidi ya Standard Liege, ameishuhudia timu yake ikishindwa kuchomoza na ushindi baada ya kuchapwa magoli 2-0 kwenye mechi iliyopigwa Stade Maurice Dufrasne.
Dakika ya 11 katika kipute hicho cha Ligi kuu ya Ubelgiji, 'Belgium Pro League' , Genk waliruhusu goli la kwanza lililofungwa na Belfodil na kudumu kwa dakika zote za kipindi cha kwanza.
Licha ya kocha wa Genk, Peter Maes kufanya mabadiliko kwa kuwatoa wachezaji watatu, Bryan Heynen na kumuingiza Susic huku Thomas Buffel akimpisha Trossard lakini bado mabadiliko hayo hayakubadili matokeo badala yake mambo yakazidi kuwa magumu.
Dakika ya 90 Genk wakaruhusu goli lingine safari hii Orlando Sa akikwamisha mpira kambani.
Genk inashika nafasi ya saba ikiwa na pointi 10 baada ya kucheza mechi sita ikishinda michezo mitatu, sare mbili na kupoteza mechi mbili.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video