Bao pekee la Farouk Miya katika dakika ya 35 limetosha kuwapelekea Uganda Cranes leo kupata tiketi ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu walipofanikiwa kufanya hivyo kwa mara ya mwisho mwaka 1978 baada ya kuwafunga Comoro bao 1-0.
Miya alifunga bao hilo baada ya kupiga shuti lililookolewa na kipa wa Comoro kabla ya Moses Oloya kuunasa na kumpasia Miya tena na kuukwamiha kimiani mpira huo.
Uganda wamefuzu kama mshindwa bora baada ya Burkina Faso kushinda 2-1 dhidi ya wageni Botswana na kuongoza kundi.
Kwa ushindi huo, Uganda inamaliza nafasi ya pili kwenye Kundi D kwa pointi zake 13, huku Burkina Faso ikiwa kileleni kwa kuwa na alama 13 wakiwa na tofauti nzuri ya magoli, Botswana ya tatu ikiwa na pointi sita wakati Comoro wakishika mkia wakiwa na alama tatu.
Mara ya mwisho The Cranes kucheza Afcon ilikuwa mwaka 1978 ilipofanikiwa kufika hadi fainali na kufungwa na Black Stars ya Ghana.
0 comments:
Post a Comment