Friday, September 16, 2016

Samuel Eto'o amemuunga mkono Xavi kwa kile alichoongea juu ya mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo.

Hivi karibuni Xavi alimuelezea Ronaldo kama mchezaji "mwenye uwezo mkubwa", lakini bado uwezo wake haukaribiani hata kidogo na ule wa Lionel Messi ambaye anakipiga Barcelona.

Maneno hayo yalisababisha Ronaldo naye ajibu mapigo ambapo alimkejeli Xavi kwa kumwambia yeye (Ronaldo) tayari ana Ballon d'Or tatu mkononi, wakati Xavi hajawahi kushinda hata mara moja, na kuongeza kuwa kiungo huyo wa zamani wa Barcelona aache kutafuta kusikika kupitia yeye.

Eto'o hakuvutiwa na meneno ya Ronaldo, na hivyo amesema kwamba ugawaji usiozingatia haki kwenye tuzo hiyo ndio sababu kubwa ya Xavi kutoshinda.

"Kama tuzo ya Ballon d'Or ingekuwa inazingatia haki, basi  Xavi angeweza kushinda mara tano au sita hivi," Eto'o alinukuliwa na gazeti la El Larguero.

"Xavi anahitaji heshima zote kubwa kwenye ulimwengu huu wa soka."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video