Sunday, September 25, 2016

Didier Drogba kwa sasa hawezi tena kuidhuru Arsenal uwanjani, lakini bado anaweza kuwafanyia hivyo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kumpa kijembe Theo Walcott kupitia Twitter.

Walcott ameendelea kuwa kwenye kiwango bora tangu msimu mpya kuanza baada ya kufunga goli moja kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya mahasimu wao Chelsea.

Baada ya mchezo huo alionesha furaha kubwa juu ya matokeo hayo na kupost picha akiwa anasherehekea iliyoambatana na ujumbe.

Hata hivyo, kupitia tweet hiyo Drogba alimjibu Walcott kwa kumpongeza kwa ushindi na kurusha kijembe cha utani kiaina.

Drogba aiandika hivi: 'Hongera sana kwa ushindi bro @theowalcott, lakini ni rahisi sana kwa panya kutawala pale paka anapokuwa hayupo'. 

Drogba anakumbukwa kwa kuwa mwiba mkali kwa Arsenal wakati akicheza Chelsea kila walipokutana, akiwa amefunga magoli 15 kwenye michezo 16 kati ya mwaka 2004 na 2012. 

Na hivi karibuni tena aliwafunga Arsenal kwa mara nyingine kwenye mchezo wa kirafiki wa pre-uliofanyika Marekani, ambapo alikuwa miongoni mwa wachezaji waliounda kikosi cha MLS All-Stars kilichofungwa mabao 3-1.

Kabla ya mchezo wa jana katika dimba la Emirates, Arsenal walikuwa wamewafunga Chelsea mara moja ndani ya miaka mitano. Hiyo ilikuwa mwaka 2011 wakati huo Cesc Fabregas alikuwa nahodha wa Arsenal.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video