Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Andre Schurrle ndiye alikuwa mwokozi wa Borussia Dortmund na kulinda rekodi yao bora nyumbani dhidi ya Real Madrid baada ya kusawazisha goli dakika ya 87 na kufanya matokeo kuwa 2-2.
Katika mchezo huo wa Champions League Kundi F uliopigwa Signal Iduna Park, Real walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Cristiano Ronaldo dakika ya 17 baada ya kuunganisha vyema pasi ya kisigizo ya Gareth Bale.
Pierre-Emerick Aubameyang aliiswazishia Dortmund baada ya kuungnisha mpira wa adhabu uliopanguliwa na kipa wa Madrid Keylor Navas kabla kumgonga beki Raphael Varane na hatimaye kumfikia Aubameyang aliyeuweka mpira huo kambani.
Raphael Varane alifuta makoa yake na kuipa Madrid goli la pili dakika ya 68 lakini hata hivyo Schurrle alisawazisha bao hilo.
Dondoo muhimu
- Katika jumla ya michezo yote 11 waliyokutana na Dortmund, Real Madrid wameshinda mara 4, sare mara 4 na wamefungwa mara 3.
- Katika michezo sita waliyokutana na Real Madrid Signal Iduna Park, Dortmund hawajafungwa hata mchezo mmoja kati ya hiyo sita, wameshinda mara 3 na kutoka sare mara 3.
- Mchezo wa mwisho kukutana kati ya hizi timu mbili kabla ya huu wa usiku wa kuamkia leo ulikuwa ni kwenye robo fainali ya Champions League msimu wa 2013/14. Real walishinda kwa wastani wa mabao 3-2. Mchezo wa kwanza Dortmund walifungwa mabao 3-0 na wao kulipiza nyumbani kwa kushinda mabao 2-0.
0 comments:
Post a Comment