
Kiungo wa zamani wa Arsenal Abou Diaby ameamua kufunguka kuhusu ya maumivu ya kisaikolojia aliyopata kutokana na kusemwa vibaya na watu juu ya majeraha yaliyokuwa yukimwandama na kuharibu kabisa maiha yake ya soka.
Diaby, ambaye alikuwa akitajwa kuwa ndiye mrithi halisi wa Patrick Vieira wakati alipopandishwa kutoka academy ya Arsenal, alitemwa na klabu hiyo msimu uliopita baada ya kucheza michezo miwili tu tangu mwaka 2013.
Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 29 kwa sasa anakipikiga kunako klabu ya Marseille ya Ufaransa, lakini amecheza mechi nne tu katika michuano yote msimu uliopita na sasa ameamua kufunguka juu ya maumivu ya kisaikolojia anayopata kutokana na hali yake.
"Wanasema mwili wangu umeundwa kwa glasi," amenukuliwa na gazeti la Daily Mail.
"Inaumiza sana hasa kisaikolojia. Watu hawajui tu namna gani napambana kila siku kwenye maisha yangu ili nirudi katika hali yangu, lakini ndiyo hivyo tena, nitafanyaje, hiyo ndiyo stori ya maisha yangu."
Diaby alicheza zaidi ya michezo 150 akiwa Arsenal lakini amekiri kwamba hakuwa kurejea katika hali yake baada ya mwaka 2006 kuvujwa mguu na mchezaji wa Sunderland Dan Smith.
"Bila shaka ni wakati ambao ulimaliza ndoto zangu zote," alisema. "Hiko ndicho chanzo ya yote haya. Ilinifanya nisiwe huru tena uwanjani kwaajili ya kujihadhari na sehemu yangu ya kifundo cha mguu (ankle) na kusababisha nisiwe tena katika kiwango bora. Kabla ya hapo nilikuwa sina matatizo ya aina ya yoyote ya misuli, maisha yangu yalikuwa mzuri kabisa."
0 comments:
Post a Comment