Saturday, September 17, 2016

Antonio Conte amepata kipigo chake cha mara ya kwanza akiwa kama bosi wa Chelsea baada ya Liverpool kuwafunga Darajani kwa mabao 2-1 na kuchupa moja kwa moja mpaka nafasi ya nne wakiwa na alama 10 sambamba na Chelsea lakini wakizidiwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Beki wa kati wa Liverpool Dejan Lovren aliifunga goli la kwanza baada ya kuuganisha krosi kutoka kwa Philippe Coutinho kutokana na mabeki wa Chelsea kuchelewa kumkaba.

Jordan Henderson, ambaye ni nahodha wa Liverpoo akaongeza la pili baada ya kuachia shuti kali ( thunderbolt) na kwenda mapumziko wakiwa na akiba ya mabao mawili mkononi.

Kipindi cha pili Chelsea waliimarika na kupata bao kupitia kwa Diego Costa ambaye aliunganisha pasi ya Nemanja Matic, lakini mpaka mwisho wa mchezo matokeo yalibaki kuwa hivyohivyo.

Liverpool wamefikisha alama 10 sambamba na Chelsea na Everton.

Vijana hao wa Jurgen Klopp pia wameshawaadhibu Arsenal na Mabingwa Watetezi Leicester,jumlisha droo dhidi ya Tottenham, huku wakipoteza mchezo mmoja tu dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu ya Burnley.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video