Dondoo muhimu
Head-to-head
- Chelsea wameifunga Liverpool mara mbili tu kwenye michezo tisa iliyopita waliyokutana kwenye dimba la Stamford Bridge (wameshinda mara 2, droo mara 3, kufungwa mara nne4).
- Hii ni mara ya 175 timu hizo zinakutana kwenye mechi za ushindani. Liverpool (wameshinda mara 75, Chelsea mara 61, droo mara 38).
Chelsea
- Endapo watashinda mchezo wa leo, Chelsea watakuwa wamepata ushindi mara tatu mfululizo kwenye Premier League katika uwanja wao wa nyumbani kwa mara ya kwanza tangu May mwaka jana.
- Aston Villa ambao walishuka daraja ndio timu pekee iliyoshinda mechi chache za nyumbani kuliko Chelsea msimu uliopita.
- Chelsea walau wamefunga magoli mawili kwenye kila mchezo kati ya michezo minne ya ufunguzi.
- Diego Costa tayari amefunga mara nne - msimu uliopita ilimchukua mpaka kipindi cha Boxing Day kufikia idadi hiyo ya magoli.
- Antonio Conte ameshinda michezo ya ligi 21iliyopita nyumbani akiwa kama meneja, na hajafungwa kwenye michezo 30 tangu Juventus ilivyofungwa na Sampdoria Januari 2013.
Liverpool
- Jumla ya idadi ya pointi 32 za Liverpool walizopata kwenye michezo 17 iliyopita inazidiwa na ile ya Manchester United tu (34).
- Endapo wataruhusu goli kwenye mchezo wa leo, watakuwa wamecheza michezo tisa ya ugenini bila clean sheet kwa mara ya kwanza tangu May 2005.
0 comments:
Post a Comment