Monday, September 12, 2016

Mario Balotelli jana amewafunga midomo mahasimu wake kwa kufunga magoli mawili kwenye mchezo wake wa kwanza kabisa kwenye timu yake ya Nice na kushinda 3-2 dhidi ya Marseille.

Baada ya kuwa na misimu miwili mibovu akiwa na Liverpool na baadaye AC Mila, Balotelli alionekana kupotea kwenye ramani ya soka.

Katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi lililofungwa hivi karibuni, Liverpool walipata tabu sana kutafuta sehemu ya kumuuza ikafikia wakati hata vilabu kutoka Serie C, India na China vikaja na ofa ya kumnunua.

Lakini Nice wakafanikiwa kumchukua, na jana sasa katika mchezo wake wa kwanza ameonesha kwamba bado ni mfumaniaji mzuri wa nyavu baada ya kuweka mbili kambani.

Baada ya Balloteli kufanya yake, Jamie Carragher aka-Tweet majungu kuhusu tukio hilo la Balotelli na hapo ndipo alipogeuziwa kibao.

Wengi waliomjibu wamemuona kama mtu mpumbavu au mjinga asiye na nidhamu kwa watu.

Carragher hajawahi kuwa shabiki wa Balotelli hata siku moja na wakati mchezaji huyo akiondoka Liverpool alimrushia maneno mengi ya kejeli.

Hii ndiyo Tweet yake


0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video