Wednesday, September 7, 2016

AZAM FC leo wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Tanzania Prisons, mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa mgumu kwa pande zote mbili kutokana na kushambuliana kwa zamu, Azam walianza kulifikia lango la timu ya Prisons mnamo dakika ya nne tu lakini kichwa cha Shomari Kapombe lakini kipa wa Prisons aliokoa hatari hiyo.

Timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu mpaka kipindi cha kwanza kinaisha, hakuna timu iliyopata goli.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ileile kwa timu zote kushambuliana kwa zamu, lakini walikuwa ni Azam ambao walipata goli dakika ya 59 baada ya kiungo wa timu hiyo Muivory Coast Kipre Bolou kupiga shuti kali lililogonga mwamba akiwa ndani ya eneo la hatari na kutinga wavuni.

Baada ya goli hilo Prisons walionekana kutulia na kushambulia kwa malengo ya kusawazisha lakini hata hivyo ukuta imara wa Azam uliokuwa ukiongozwa na Amoah pamoja na Mwantika uliondoa hatari zote na kufanya matokeo kubaki 1-0.

Kwa matokeo hayo, Azam wanafikisha pointi 7 baada ya kucheza michezo mitatu sambamba na Simba na Mbeya City lakini timu zote zikitofautiana kwa wastani wa magoli ya kufunga na kufungwa.


0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video