![]() |
Adam Lallana akishangilia bao lake |
Kocha mpya wa Timu ya soka ya England, Sam Allardyce, maarufu kwa jina la 'Big Sam' ameanza vyema kazi yake baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Slovakia kwenye mechi ya kuwania kufuzu kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi iliyopigwa uwanja wa Antona Malatinskeho mjini Trnava .

Shukrani pekee zimwendee Adam Lallana aliyefunga bao pekee kwa kikosi cha Allardyce.
Baada ya ushindi huo, msimamo wa kundi F unaonekana hivi.

Alladryce alionekana mwenye furaha zaidi (pichani chini) kufuatia kuibuka kidedea kwenye mtanange wake wa kwanza.

Waswahili husema mwanzo mzuri mwisho huwa mzuri, ingawa sio lazima iwe hivyo kwani inaweza kuwa mwanzo mzuri mwisho mbaya au mwanzo mbaya mwisho mzuri.

0 comments:
Post a Comment