Beki wa kulia wa PSG Serge Aurier amehukumiwa kutumikia kifungo cha miezi miwili baada ya kutuhumiwa kumshambulia ofisa wa polisi jijini Paris.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ,23, ametuhumiwa kwa kitendo cha kumpiga kiwiko kifuani ofisa huyo wa polisi baada ya kuwambiwa kuchukuliwa kipimo cha breath test mwezi May mwaka huu.
Aurier kwa upande wake amesema alifanya hvyo baada ya kufanyiwa kitendo kisicho cha kiungwa na na polisi huyo huku taarifa zikieleza Muivory Coast huyo anayo fursa ya kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.
Mbali na adhabu hiyo pia amepigwa faini ya euro 600 na mahakama na zinaweza kuongezeka euro 1,500.
“Ulikuwa ni ukatili,” Aurier alisema kwenye moja ya runinga za nchini Ufaransa wakati akihojiwa mwezi June. “Maofisa wa polisi walitoka nje ya nje ya gari na kuanza kunitukana na kunifanyia ukatili brutalised hadi kuniumiza sehemu ya mdomo wangu.
“Na kitu kibaya zaidi ni kitendo cha moja ya maafisa wa polisi kusema kwamba nilimpiga kiwiko kifuani. Kama ningetaka hata kumgusa, ningeweza kumsukuma mbali. Lakini yeye alinibugudhi na alinisukuma mara kadhaa usoni.
“Sina kitu cha kuficha katika hii kesi, kuna mashahidi kama watano au sita hivi ambao wamesema hivyo hivyo kama nilivyosema mimi.”
Hata hivyo mchezaji huyo anatarajiwa kuwemo katika kikosi cha PSG kitakachocheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Jumatano dhidi ya Ludogorets.
Mpaka sasa ameshaichezea PSG mechi 5 msimu huu na kutoa pasi ya goli kwa Edinson Cavani katika mechi dhidi ya Arsenal, wiki mbili zilizopita.
0 comments:
Post a Comment