Leo usiku Wayne Rooney anaenda kuweka rekodi mpya pale England itakapovaana na Slovakia katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 utakaochezwa majira ya 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Rooney anaenda kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi kuwahi kutokea katika Timu ya Taifa ya England.
Kabla ya mchezo huu wa leo, Rooney anafungana na David Beckham wote wakiwa wamecheza michezo 115.
Zaidi ya hapo, Rooney pia anashikilia rekodi ya mfungaji bora wa muda wote kwenye taifa hilo.
Ikumbukwe kuwa, hivi karibuni Allan Shearer alinukuliwa akisema ni wakati wa Rooney sasa kujiengua England na kuwaachia vijana, hali iliyopingwa vikali na Rio Ferdinand ambaye alisisitiza Rooney aendelee kubaki ili kutoa uzoefu zaidi kwa vijana.
Hivyo kuelekea mchezo huo, David Beckham amemimina pongezi kwa nahodha huyo wa England kwa mafanikio hayo makubwa anayoenda kuyapata.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Beckham ameandika hivi:
"So tonight Wayne becomes England's most capped outfield player .. I keep listening to people say Wayne should stop playing for his country to prolong his club career .. Wayne should retire from playing for his country... Seriously .. As a player you retire when you're ready.. Representing you're country is the highest level you can reach as a professional player , walking out in an England shirt at Wembley is one of the greatest feelings as a player you can ever have... Don't let anyone take that away from you .. Every kid around the world that loves this game dreams of walking out in the national team colours and representing the country they love .. Continue till you can't give anymore .. Congratulations mate 🇬🇧 @manchesterunited @england
Kwa kiswahili
"Kwa hiyo leo Wayne anakuwa mchezaji aliyeichea England mechi nyingi zaidi kwa wachezaji wa ndani.. Nimejaribu kwasikiliza watu wanaosema eti ni muda mwafaka kwa Wayne kuacha kuitumikia nchi yake ili aelekeze nguvu zote kwenye klabu yake..hivi kweli wako serious wanasema Wayne astaafu kulitumikia taifa lake...Ukiwa kama mchezaji unapaswa kustaafu unapokuwa tayari kufanya hivyo. Kuwakilisha nchini yako ni level ya juu kabisa kwa mchezaji mwenye weledi, kuvaa jezi ya England tena ikiwa inacheza Wembley ni fahari kubwa ukiwa kama mchezaji unayejitambua...Usijaribu kumsikiliza yeyote anayeweza kukulghai kuacha kufanya hivyo...Kila mtoto ulimwenguni kote ambaye anapenda huu mchezo anaota siku moja kuwa katika jezi ya taifa lake na kuliwakilisha katika michuano mbalimbali...Endelea na uzi huo huo mpaka itakapofikia ukomo wa nguvu zako...Hongera sana ndugu yangu 🇬🇧 @manchesterunited @england"
0 comments:
Post a Comment