Barcelona ameshindwa kupunguza pengo la pointi dhidi ya wapinzani wao wakubwa ambao ndio vinara wa La Liga Real Madrid kufuatia kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya wabishi wa Atletico Madrid, mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Camp Nou
Baada ya kushindwa kupenya ngome ya Atletico kwa njia ya kupiga pasi nyingi, Barca waliamua kutumia mpira mirefu na ndipo walipofanikiwa kupata bao kupitia kwa Ivan Rakitic kufuatia krosi safi ya Andres Iniesta.
Dakika ya 59 Barcelona walipata pigo baada ya Lionel Messi kupata majeraha na nafasi yake kuchukuliwa na Arda Turan.
Atletico waliitumia vizuri faida ya kutoka kwa Messi kwa kijipatia bao dakika ya 61 kupitia kwa Angel Correa baada ya kuwahadaa mabeki wa Barcelona.
Gerard Pique na Diego Godin kwa nyakati tofauti walijaribu kuzipatia timu zao mabao lakini juhudi zao hazikuzaa matunda.
Bado haijathibitishwa kwamba majeraha ya Messi ni makubwa kiasi gani na atakaa nje kwa muda gani.
0 comments:
Post a Comment