Arsene Wenger amekataa kujibu kauli ya hasimu wake Jose Mourinho kwamba siku moja angemharibu sura yake
Katika toleo la nne la kitabu cha ‘Jose Mourinho: Up Close and Personal’, Daily Mail imechapisha maneno ya Mourinho akisema alitaka kumharibu sura Arsene Wenger wakati akiwa meneja wa Chelsea msimu wa 2013-14
Akiongea kuelekea mchezo wa London derby dhidi ya Chelsea, Wenger amekataa kuzungumza chochote juu ya kauli hiyo ya Wenger.
“Sijasoma kitabu na hata hivyo sidhani kama nitakisoma,” aliwaamba wanahabari. “Sina cha kusema juu ya kauli hiyo.
“Mimi naongea kuhusu masuala ya soka tu. Mimi si mtu wa mrengo wa kuharibu mambo, nasema kamwe. Siku zote mimi ni mtu wa kujenga tu na siwezi kuongea chochote kuhusu hilo.
“Akili yangu yote inawaza kuhusu mchezo wa kesho na namna tutakavyoweza kucheza ili kupata matokeo.
“Sina matatizo binafsi na mtu yeyote yule. Namheshimu kila mtu katika tasnia yetu na sidhani kama ni vizuri sana kuzungumzia masuala ya timu nyingine.
“Uhasama binafsi ambao mnaousema haukuwa kwenye akili yangu. Kitu muhimu cha kuangalia ni kwamba tunaenda kucheza mchezo mkubwa wenye hisia kubwa.
Wenger anasherehekea maadhimisho ya miaka 20 ya muda wake aliotumikia Arsenal na endapo atashinda mchezo wa kesho dhidi ya Chelsea, basi furaha yake itakuwa mara mbili zaidi.
0 comments:
Post a Comment