MAAFANDE wa JKT Ruvu Stars baada kuahirishwa kwa mchezo wao dhidi ya
Mabingwa Watetezi Yanga SC uliotakiwa kuchezwa Jana uwanja wa Taifa, Dar es
salaam, hivi sasa wameelekeza nguvu zao kwenye mechi ya mwishoni mwa Juma hili ambapo
wataikabili African Lyon Uwanja wa
Mabatani, Mlandizi, Pwani.
Msemaji wa JKT Ruvu, Afisa Mteule Daraja la Pili, Constantine Masanja
amesema: “Hivi sasa timu inaendelea na mazoezi katika kambi ya JKT Mbweni chini
ya kocha mkuu Comred Denis Malale Hamsini”.
Aidha, Masanja ameeleza kuwa wachezaji wanne waliokuwa kwenye Mashindano
ya Majeshi kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyomalizika
mwezi uliopita Kigali, Rwanda, watajiunga na kambi wakati wowote.
Wachezaji hao ni Paul Mhadize, Hamis Seif, Emmanuel Pius na Juma Mussa Kiumbu.
0 comments:
Post a Comment