Monday, September 12, 2016

Kiungo wa Manchester United Paul Pogba amekuwa akikosolewa sana juu ya kiwango alichokionesha kwenye mchezo dhidi ya mahasimu wao Manchester City hali iliyopelekea kupoteza kwa magoli 2-1 kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Lakini inaonekana kama vile kosa si lake bali la meneja wake Jose Mourinho ambaye alishindwa kumtumia vizuri baada ya kumchezesha kiungo cha chini badala ya juu hali iliyowapa City fursa kubwa ya kutawala eneo la kiungo.

Akiwa ametoka kuvunja rekodi ya usajili duniani kwenye dirisha lililofungwa hivi karibuni, Pogba ameonekana kuguswa na matokeo hayo.

Kupitia kwenye akaunti yake ya Instagram, Pogba ameonesha kusikitishwa na matokeo hayo dhidi ya mahasimu wao na kuamua kuandika ujumbe mfupi wenye maana pana sana.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa ameandika hivi: “The season is just starting, we don’t lose, we learn. United we stand”.

Akimaanisha kwamba: "Msimu ndiyo kwanza unaanza, huwa hatupotezi bali tunajifunza. Unite hatuyumbi."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video