Thursday, September 1, 2016

 Wakati Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania, Taifa Stars,  ikitarajia kwenda Nigeria kuikabili Timu ya Taifa ya nchi hiyo, Super Eagles,  Septemba 3 mwaka huu katika mechi ya kukamilisha ratiba ya kuwania nafasi ya kucheza fainali za kombe la Mataifa ya Afrika,  AFCON 2017 mwakani nchini Gabon, ligi kuu ya kandanda Tanzania Bara itaendelea kama kawaida Mwishoni mwa Juma hili.
Kituo pekee chenye haki ya kurusha Live mechi za Ligi kuu, Azam TV,  kimetoa ratiba yake ya mechi zitakazokuwa Live mwishoni mwa Juma hili na katikati ya Wiki Ijayo.
Jumamosi, Mtanange wa Mbao FC dhidi ya Mbeya City utakuwa Live kupitia Azam TWO na Azam Sports HD kuanzia Saa 10:00 Jioni.
 Jumapili Kipute cha Stand United na Toto African kitakuwa Live Azam TWO kuanzia saa 10:00 Jioni.
 Septemba 7 mwaka huu, Tanzania Prisons na Azam FC, mechi itakuwa Live kupitia Azam Sports HD kuanzia saa 10:00 Jioni.
Uwanja wa Uhuru Dar Es Salaam, Simba na Ruvu Shooting wataonekana Live kupitia Azam TWO kuanzia saa 10:00 Jioni.
Ukiachana na mechi hizo zitakazokuwa Live kupitia Azam TV, Ratiba ya VPL inaonesha Wikiendi hii kutakuwa na mitanange mingine kama ifuatavyo:

Septemba 3 mwaka huu:

 Kagera Sugar vs Mwadui FC-Uwanja wa Kaitaba
Maji Maji FC vs Mtibwa Sugar-Uwanja wa Maji Maji Songea
JKT Ruvu Stars vs African Lyon-Uwanja wa Mabatini

Mechi nyingine itapigwa Septemba 7 Mwaka huu Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara kati ya wenyeji Ndanda FC na Mabingwa watetezi, Young Africans.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video