Arsene Wenger amekiri kwamba mshindi katika mchezo wa derby ya Manchester kesho atakuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa Premier League.
Manchester United na Manchester City wote mpaka sasa wamejikusanyia alama tisa baada ya kucheza mechi tatu wakiwa chini ya utawala mpya wa mameneja Jose Mourinho na Pep Guardiola.
Arsenal kwa upande wao wana alama nne hivyo kuachwa nyuma alama tano dhidi ya miamba hiyo
'Timu hizi mbili zimeanza ligi vizuri, hivyo timu itakayoshinda itajiwekea mazingira mazuri ya kisaikolojia kuliko kimahesabu,' Wenger alisema
.
'Unaweza kusema kwamba timu itakayoshinda kesho basi moja kwa moja itahusishwa na kutwaa taji la Premier League itakapofika mwezi Mei mwakani. Ni mapema kidogo. Lakini utakuwa ni mchezo mzuri sana kuuangalia.'
'Nitautazama mchezo huo na kuangalia kidogo ubora na udhaifu wao,' alisema. 'Zaidi ni kuhusu kiwango chao watakachokionesha uwanjani na hicho ndicho kitakachoamua matokeo ya mchezo.
0 comments:
Post a Comment