Wednesday, September 28, 2016

Arsenal wanaingia dimbani kusaka ushindi wa kwanza wakiwa nyumbanin kwenye mchezo wa Kundi A katika Michuano ya UEFA msimu huu kufuatia mchezo wa awali kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya PSG ya Ufaransa, mchezo uliofanyika Parc des Princes jijini Paris. 

Arsenal watamkosa kiungo wao mahiri mkabaji Francis Coquelin kufuatia kupata jeraha la goti katika mchezo dhidi ya Chelsea uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, wakati waliposhinda mabao 3-0.

Granit Xhaka atachukua nafasi ya kiungo huyo raia wa Ufaransa, nafasi ambayo ni adhimu kwake kutokana na kukutana na kaka yake vilevile timu yake aliyojifunzia kucheza soka.

"Vipimo vinaonesha kwamba hajapata maumivu makubwa sana. Nadhani atakuwa nje kwa wiki tatu hivi," Wenger amesema.

Majeraha ya Coquelin yatamfanya kukosa michezo ya ligi dhidi ya Burnley na Swansea na pengine pia mchezo mwingine wa Champions League dhidi ya Ludogorets Razgrad Oktoba 19.

Mshambuliaji Olivier Giroud pia ataukosa mchezo wa leo kutokana na kuendelea kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopata kwenye mchezo wa awali dhidi ya PSG.

Akigusia mchezo uliopita dhidi ya Chelsea, Wenger amesema: "Tulikuwa na mchezo mzuri sana Jumapili lakini inabidi tuoneshe hivi tena kwenye michezo ijayo ili kuwapa faraja mashabiki wetu.

"Kilichonifurahisha sana ni wachezaji kucheza kwa nguvu, kutokuwa na hofu bila kujali chochote ambacho kingetokea, walicheza kwa nidhamu kwa ushirikiano wa hali ya juu. Hiyo ni dalili nzuri sana.

Dondoo muhimu


  • Basel wameshinda michezo yote tisa waliyocheza kwenye ligi yao (Swiss Super League) mpaka sasa msimu huu, wakiwa wamefunga mabao 27 na kuruhusu mabao 7 tu kugusa nyavu zao.
  • Katika mchezo uliopita wa Champions League dhidi ya Ludogrets walilazimishwa sare ya bao 1-1.
  • Arsenal hawajawahi kupoteza mchezo dhidi ya timu yoyote ya Uswisi kwenye michezo minne waliyocheza, wakifunga mara nane na kuruhusu bao mara moja tu.
  • Basel wameshinda mchezo mmoja tu kati ya 11 iliyopita waliyocheza nchini England, wakati walipoifunga Chelsea 2-1 katika Uwanja wa Stamford Bridge mwaka 2013.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video