Yanga SC leo ipo ugenini mkoani Mtwara kukabiliana na wenyeji wao Ndanda FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaofanyika kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Katika mchezo wa leo, Yanga itawakosa baadhi ya wachezaji wake kutokana na sababu mbalimbali kama vile matatizo ya kifamilia na kuchelewa kurudu kambini kutokana na kuwa na majukumu ya kuyatumikia mataifa yao katika mechi za kimataifa.
Kuelekea mchezo huo kikosi cha Yanga kitakuwa kama ifuatavyo;
Kikosi kinachoanza: Ali Mustafa, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Andrew Vicent, Nadir Haroub, Thabani Kamusoko, Saimoni Msuva, Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Obrey Chirwa na Deusi Kaseke
Akiba: Beno Kakolanya, Hassani Kessy, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Juma Mahadhi, Mateo Antony na Yussuf Mhilu
0 comments:
Post a Comment