Manchester City chini ya Pep Guardiola wameanza kampeni yao ya Ligi ya Mabingwa vizuri baada ya kuwachapa Wajerumani wa Borussia Moenchengladbach mabao 4-1, katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Etihad.
Sergio Aguero ndiyo shujaa wa mchezo huo baada ya kufunga magoli matatu (hat-trick) na kupeleka kilio kwa Wajerumani hao.
Aguero alifunga magoli hayo mnamo dakika za 9, 27 na 77 huku kinda wa timu hiyo Mnigeria Kelechi Iheanacho akimalizia msumari wa mwisho mnamo dakika ya 90.
Kwa mara ya kwanza tangu asajiliwe kutoka Borussia Dortmund, kiungo wa Kimataifa wa Ujerumani Ilkay Gundogan alicheza baada ya kupona majeraha yake.
City walianzisha kikosi kile kile kilichoanza dhidi ya United wikiendi iliyopita isipokuwa David Silva, ambaye alipumzishwa kutokana na kutokuwa fiti kwa asilimia mia moja na ndipo pengo lake likazibwa na Ilkay Gundogan.
Kauli ya Pep Guardiola baada ya mchezo
"Shukrani za dhati ziende kwa wachezaji wote kwa kunipa furaha mimi na mashabiki pia. Natumaini mpira wetu utaendelea kuimarika siku hadi siku na mashabiki wote watafurahia kutuangalia. Tunahitaji sapoti kubwa kwa mashabiki kujaza uwanja ili kushindana na walio bora.
"Mpaka sasa tumeshacheza michezo kadhaa rasmi na tumefanikiwa kushinda yote. Tunazidi kukmarika siku hadi siku. Leo (jana) tumezidi kujifunza mengi zaidi. Isipokuwa kwenye dakika 15 za mwisho za kipindi cha kwanza, lakini vinginevyo tuliutawala mchezo kwa asilimia kubwa sana."

0 comments:
Post a Comment