Thursday, August 4, 2016


Unamkumbuka yule winga Mganda aliyeshindwa kutamba akiichezea kwa muda mfupi klabu ya Simba?
Namzungumzia Brian Erick Majwega ambaye baada ya kushindwa kutamba nchini Tanzania, sasa anakipiga KCCA ya nchini kwake.
Nyota huyo wa zamani wa Azam FC amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Soka ya Uganda, The Cranes' kinachojiandaa kufanya ziara maalum kanda za Mikoa ya nchi ya Uganda.
kocha mkuu wa Uganda, Milutin ‘Micho’ Sredejovic ameita kikosi cha nguvu ambacho Kesho kutwa (Agosti 6) kitacheza mechi ya kirafiki kwenye uwanja wa Masaka Recreational kuanzia majira ya saa 10:00 jioni.
Micho alitangaza kikosi chake katika mkutano wa kila wiki wa FUFA na waandishi wa habari ambao hufanyika Jenjo la FUFA lililopo Mengo, Mjini Kampala.
Mkufunzi huyo wa zamani wa Yanga sc na timu ya Taifa ya kandanda ya Burundi, amechanganya damu changa na wakongwe ili kuwapa nafasi wachezaji wote anaoona wanaweza kuisaidia nchi yake.
Wachezaji wengine waliorejea kwenye kikosi ukiachana na Majegwa ni Geoffrey Sserunkuma, Vincent Walugembe Kayizzi na Mike Sserumaga.
Hassan Wasswa Mawanda ndiye nahodha, wakati beki wa kati wa Simba, Juuko Murishid na aliyekuwa mshambuliaji wa kikosi cha Msimbazi, Hamis Kiiza wakikosekana katika kikosi hicho.
Kikosi kamili cha Uganda Cranes :
Magolikipa: Benjamin Ochan (KCCA) and Yasin Mugabi (SC Villa)
Walinzi: Nicholas Wadada (Vipers), Joseph Nsubuga (SC Villa), Hassan Musana (Bul), Hassan Wasswa Mawanda (Captain) - Al Shorta, Iraq, Rashid Toha (Onduparaka), Timothy Awanyi (KCCA), Halid Lwaliwa (Vipers), Bernard Muwanga (SC Villa)
Viungo: Ivan Ntege (KCCA), Kezironi Kizito (Vipers), Mike Sserumaga (SC Villa), Vincent Kayizzi (KCCA), Abdumalik Tabu (SC Villa), Martin Kizza (SC Villa) and Brian Majwega (KCCA)
Washambulaiji: Geoffrey Sserunkuma (KCCA), Erisa Ssekisambu (Vipers), Shaban Muhammed (Onduparaka), Musa Esenu (Soana), Edrisa Lubega (Proline)
Mchezaji anayecheza nje: Sulaiman Luzige (Vaxjo, Sweden)

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video