Tuesday, August 23, 2016

Mchezo wa mwisho wa Kundi A michuano ya kombe la Shirikisho Afrika kati ya TP Mazembe dhidi ya Yanga umemalizika kwa Yanga kukubali kichapo cha magoli 3-1 ikiwa ugenini na kuendeleza rekodi yake ya kutoshinda michezo yake mitatu ya hatua ya nane bora msimu huu.

Bolingi alianza kuifungia Mazembe bao la kwanza dakika ya 28 kipindi cha kwanza.
Yanga ilipata pigo dakika mbili baada ya kuruhusu goli, Andrew Vicent ‘Dante’ alioneshwa kadi nyekundu na kuiacha Yanga ikicheza pungufu kwa dakika zote zilizobaki.

Dakika 11 baada ya kipindi cha pili kuanza, Rainford Kalaba aliifungia Mazembe bao la pili kabla kuongeza bao lake la pili likiwa ni bao la tatu kwa Mazembe mnamo dakika ya 64.


Amis Tambe aliifungia Yanga bao pekee akiunganisha mpira uliogonga ‘mtambaa panya’ baada ya Haruna Niyonzima kupiga mpira wa adhabu ndogo.

Matokeo hayo yanaipa Mazembe fursa ya kuongoza Kundi A kwa pointi 13 ikifatiwa na Bejaia yenye pointi 8 baada ya kuichapa Medeama kwenye mchezo wake wa mwisho. Bejaia na Medeama zimefungana kwa kila kitu kwahiyo kanuni iliyotumika kuipeleka mbele Bejaia ni ile ya kuangalia matokeo ya timu hizo zilipokutana zenyewe kwa zenyewe (head-to-head).


Ikumbukwe mechi ya kwanza iliyozikutanisha timu hizo zilitoka sare (Medeama 0-0 MO Bejaia) mchezo wa pili (leo) MO Bejaia 1-0 Medeama).

Yanga  imemaliza ikiwa nafasi ya nne (yamwisho) kwenye Kundi A ikiwa na pointi nne baada ya kupata ushindi katika mechi moja (Yanga 1-0 MO Bejaia) sare moja (Yanga 1-1 Medeama) huku mechi nyingine nne ikiwa imepoteza. (MO Bejaia 1-0 Yanga, Yanga 0-1 TP Mazembe, Medeama 3-1 Yanga, Mazembe 3-1 Yanga).
Yanga imefungwa jumla ya magoli 9 huku yenyewe ikiwa imefunga magoli manne katika mechi zote 6 ilizocheza.


Kwahiyo, TP Mazembe na MO Bejaia zinafuzu hatua ya nusu fainali ya kombe ka shirikisho Afrika na kuziacha Medeama na Yanga kutoka Kundi A.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video