Saturday, August 13, 2016

YANGA SC imefufua matumaini ya kusonga mbele hatua ya nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya MO Bejaia ya Algeria katika mchezo wa marudiano Kundi A uliopigwa  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Bao pekee la Yanga limefungwa mapema dakika ya 3'  na Amissi Tambwe kutokana na piga nikupige iliyotokea langoni mwa MO Bejaia kufuatia mpira wa adhabu ndogo uliochongwa nje kidogo ya eneo la 18 na Juma Abdul na mabeki wa timu hiyo ya Algeria wakajichanganya wenyewe.
Kipindi cha kwanza: Yanga walifanya mashambulizi mengi na kumiliki kandanda kuliko MO Bejaia ambapo Takwimu kwa mujibu wa ZBC2 walioonesha Live mechi hiyo zilithibitisha kama ifuatavyo:
Yanga walipiga mashuti manne yaliyolenga lango (Shots on Target) wakati MO Bejaia  walipiga matatu.
Mashuti ambayo hayakulenga lango (Shots off Target) Yanga walipiga 9 na MO Bejaia walipiga 7.
Kwa upande wa kona, Yanga hawakufanikiwa kupata kona kipindi cha kwanza wakati wapinzani wao walipiga kona 2.
Yanga walifanya madhambi mara 8 wakati Bejaia walifanya mara 10.
Pia Yanga waliotea mara 2, MO Bejaia hawakuotea kutokana na kuwa makini zaidi.
Hakuna timu iliyopata kadi ya njano wala nyekundu katika kipindi hicho  cha kwanza, wakati hali ya Umiliki wa mpira (Ball Possession)  Yanga walikuwa mbele kwa 51% kwa 49% za MO Bejaia.

TAKWIMU ZA DAKIKA ZOTE 90 (FULL TIME)
Kabla ya ushindi wa leo, Yanga walikuwa wamepoteza mechi tatu na kutoa sare moja kwenye mechi nne walizocheza kama matokeo yanavyoonesha hapo chini:


Yanga wamefikisha pointi 4 baada ya kushinda mechi moja, sare moja na kupoteza mechi tatu kati ya hizo tano walizocheza mpaka sasa, lakini bado wanaburuza mkia.
Mechi za raundi ya mwisho ya sita zitachezwa Agosti 23 mwaka huu ambapo Young Africans waliopo kundi A watakaribishwa na TP Mazembe mjini Lubumbashi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
MSIMAMO WA MAKUNDI A NA B
Medeama SC kesho wakiwa katika ardhi yao watacheza mechi yao ya tano dhidi ya TP Mazembe ambao kiuhalisia ukitazama pointi zao kwenye msimamo hapo juu wameshafuzu hatua ya nusu fainali.
Medeama endapo wakifungwa kesho wataiongezea Yanga matumaini ya kusonga mbele, lakini itagemeana na matokeo watakayopata dhidi ya TP Mazembe.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video