Wednesday, August 17, 2016

YANGA SC na Azam fc leo wanakutana uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kucheza mechi ya Ngao ya Jamii inayoashiria kufunguliwa rasmi kwa msimu mpya wa mashindano Tanzania bara.
Yanga ambao upande wa uongozi kwa sasa hakujatulia kutokana na taarifa za mwenyekiti wao, Yusuf Manji kutaka kujiuzulu nafasi hiyo, kikosi chao kilikuwa kikifanyamazoezi katika Uwanja wa Gymkhan jijini Dar es Salaam wakati Azam FC wao jkama kawaida walijichimbia Uwanja wao wa Azam Complex nje kidogo ya Dar es Salaam.
Miamba hiyo ya soka ambayo miaka ya karibuni imekuwa na ushindani mkubwa itakutana kutokana na Yanga kuwa bingwa wa Ligi kuu Bara wakati Azam ilishika nafasi ya pili katika Kombe la Azam Sports Federation Cup, hivyo kwa kuwa kanuni inataka bingwa wa FA na ligi kuu kukutana ilibidi Yanga icheze na Azam kwa kuwa Yanga pia ilichukua ubingwa wa FA.

Kila upande unaonekana kuwa fiti kwa mchezo huo japokuwa Yanga itakuwa na wachezaji kadhaa majeruhi ambao watakosekana katika mchezo huo baadhi yao ni Geofrey Mwashiuya, Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Wakati huo huo, watu wengi wamekuwa wakiuliza ni Chaneli gani itarusha Live mechi hii ya leo.

Habari rasmi ni kuwa  KITUO cha Luninga cha Agape Television Network (ATN) kimepata haki ya kuonesha moja kwa moja mchezo huo utakaoanzia saa 10 jioni.
Mkurugenzi wa michezo wa ATN Denis Msemwa alisema wamejipanga kurusha mchezo huo ambao utakuwa na muonekano bora yaani HD huku matukio yote muhimu yakionekana.
Aidha Msemwa alisema pia vyombo vyingine vya habari vitaruhusiwa kurekodi dakika 15 za mwanzo na 15 za mwisho ili kuweza kutumia katika taarifa za habari ila baada ya mchezo wanaweza kupata CD ya mechi nzima.
Kwa upande wake Afisa Habari wa TFF,  Alfred Lucas alisema endapo mchezaji ataonywa kwa kadi katika mchezo huo adhabu hiyo itaendelea hadi kwenye mechi za ligi kuu kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu ya Vodacom.
"Kama mnakumbuka mchezaji Erasto Nyoni alioneshwa kadi ya njano katika mchezo kama huu mwaka jana ikaigharimu Azam hadi kupokwa alama kwahiyo wachezaji wanatakiwa wawe makini,"alisema Lucas.
Viingilio katika mchezo huo vitakuwa kama ifuatavyo;VIP A 20,000,VIP B na C itakuwa 15,000 huku mzunguko ikiwa ni 5,000.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video