Monday, August 1, 2016

Wakati wa Michuano ya Euro mwaka huu iliyofanyika nchini Ufaransa, Pogba alikuwa mchezaji muhimu sana kwa taifa la Ufaransa lakini allishindwa kuwapa ubingwa baada ya kufungwa na Ureno kwenye mchezo wa fainali. Lawama nyingi zilimiminwa kwake lakini Arsene Wenger ni moja ya watu waliomtetea.
Wenger alisema kwamba wakati Pogba akielekea kuwa mchezaji wa kiwango cha juu zaidi duniani, lakini imekuwa mapema mno kwa kiungo huyo kutawala medani za kimataifa.

Aufananisha usajili wa Pogba na matumizi mabovu ya fedha
Wakati wa kuelekea mchezo wa kirafiki katika ya Arsenal na Chivas Guadalajara mapema leo asubuhi, Wenger amezungumzia kwa mara nyingine suala la usajili wa Pogba.

Saga la Pogba limezidi kugonga vichwa vya habari mbalimbali kutokana na kutajwa kuwa mbioni kusajiliwa kwa ada ya uhamisho itakayovunja rekodi ya dunia kutoka Juventus kwenda Manchester United.

Wenger amesema: “Ni suala la ajabu kama huwezi kulipa kiasi hicho. Lakini kama unaweza kulipa unaweza kutolea uchanganuzi. Ni suala la kustaajabisha hasa ukifafananisha na maisha ya kawaida. Huo ndiyo ukweli halisi. Lakini tunaishi kwenye ulimwengu ambao kila shughuli ambayo inahusisha ulimwengu kwa ujumla ina pesa nyingi sana.  Mchezo wa soka umekuwa una ushindani ulimwenguni kote na ndiyo maana vilabu mbalimbali vnaweza kufanya hivyo.”

"Inaweza kuingia akilini mwako kwamba mchezaji anaweza kurudisha pesa zote hizo? Hakuna anayeweza kukokotoa hilo. Na kwasababu ni niko katika tasnia hii, mara nyingine nimekuwa nikifikiri kwamba rekodi haiwezi kwenda mbali kiasi hiko lakini kumbe sikuwa sahihi. Pengine miaka michache ijayo itakuwa 200, 300, nani anajua hilo?”

Paul Pogba anatarajiwa kusaini mkataba wa kiutumikia Manchester United  katika siku zijazo, baada ya kuwa tetesi kwa kmuda mrefu. 

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video