Beki kisiki wa Azam FC, maarufu kwa jina la Waziri wa Ulinzi, Serge Pascal Wawa amerejea na kuanza mazoezi mepesi ya Gym chini ya uangalizi wa Mtaalamu wa Viungo wa timu hiyo, Sergio Perez Soto.
Wawa alikuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili akisumbuliwa na majeraha ya goti na sasa amemepata ahueni ambapo alianza kujifua mdogo mdogo Jana asubuhi.
Wawa amekuja kivingine, safari hii amerudia mtindo wa nywele aliokuwa akiutumia wakati anacheza El Merreikh ya Sudan kabla ya kujiunga na Azam FC.
Alipoulizwa kwanini amerudia Mtindo huo wa Nywele, alijibu.
"Muonekano huu!!...nadhani nimeweka muonekano huu kwasababu wakati nacheza Sudan niliutumia, nilicheza vizuri na watu walinipenda sana, nimeamua kuuweka muonekano huu hapa".
Ni mimi Pascal Wawa, Mashabiki wa Azam nawaambia narudi, nawashukuru, mmekuwa mkija kuniona kila mara, nasema narudi, aaaaah!"
0 comments:
Post a Comment