Thursday, August 11, 2016

Mabingwa wa Soka Tanzania bara, Jumamosi ya Juma hili, uwanja wa Taifa Dar es salaam watacheza na MO Bejaia ya Algeria katika mchezo wa nne wa hatua ya Nane Bora kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika. 
Taarifa njema kwa wapenzi wa Yanga na wadau wa soka nchini ni kwamba AZAM TV kupitia Ukurasa wake rasmi wa facebook imethibitisha kwamba itarusha Live mechi hiyo.

Japo haijaelezwa ni Chaneli gani itarusha mechi hiyo, lakini taarifa zinaeleza kwamba ni kupitia Chaneli namba mbili ya Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC2) inayopatikana kwenye king'amuzi cha AZAM TV.
Licha ya kwamba Young Africans kuwa na pointi moja, bado ina nafasi ya kushika nafasi za juu katika kundi la A ambalo msimamo wake unaongozwa na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), huku Mo Bajaia ya Algeria na Medeama ya Ghana, zina pointi tano kila moja. Wakati Young Africans wanacheza na Mo Bajaia iliyoshinda mchezo wa kwanza huko Algeria, Medeama itakipiga na TP Mazembe.
 Mchezo wa Young Africans dhidi ya Mo Bajaia utachezeshwa na waamuzi kutoka Ethiopia ambako katikati atakuwa Bamlak Tessema Weyesa akisaidiwa na Kindie Mussie mstari upande wa kusini na Temesgin Samuel Atango katika mstari wa Kaskazini upande wa wakati Mwamuzi wa Akiba atakuwa Haileyesus Bezezew Belete.
Kamishna wa mchezo atakuwa Gaspard Kayijuka kutoka Rwanda wakati Desire Gahuka wa Burundi atasimamia ufanisi wa waamuzi wa mchezo na Mratibu Mkuu wa mchezo atakuwa Isam Shaaban kutoka Sudan. Mratibu huyo anatarajiwa kuwasili leo Agosti 10, 2016 wakati waamuzi watatua kesho Agosti 11, 2016 na msimamizi wa waamuzi atatua Ijumaa Agosti 12, 2016.

Kiingilio katika mchezo huo kitakuwa ni Sh 3,000 kwa mzungunguko kwa maana ya viti vya kijani, bluu na chungwa wakati Viti Maalumu vyenye hadhi ya daraja B na C kiingilio kitakuwa Sh 10,000 wakati A kiingilio kitakuwa ni Sh 15,000 kwa mujibu wa Waratibu wa Young Africans.
Mechi ya kwanza iliyochezwa nchini Algeria, Yanga ilikubali kichapo cha 1-0 kutoka kwa MO Bejaia.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video