Nemanja Vidic amesisitiza kwamba Fernando Torres sio mshambuliaji aliyewahi kumpa wakati mgumu zaidi licha ya mara kadhaa kumsumbua pindi alipokutana naye.
Legend huyo wa Manchester United amesema kwamba mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba ndiye mchezaji pekee ambaye alikuwa akimwogopa pindi timu zao zinapokutana.
Amefichua kwamba wakati Torres alikuwa akitumia mbinu zaidi kuwasumbua mabeki na kufunga muda wowote, lakini amekiri kwamba uchezaji wa Drogba ni mgumu zaidi kumkaba
Torres anakumbukuwa zaidi na Vidic kwa kila alichomfanyia wakati Liverpool ikiibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Man United katika dimba la Old Trafford mwaka 2009.
Katika mchezo huo Torres alisababisha Vidic kupewa kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi mara mbili kwa nyakati tofauti.
Lakini wakati akielelezea ubora wa Torres na Drogba, Vidic anasisitiza kwamba pia amekutana na Luis Suarez na Sergio Aguero
Akiongea na mtandao wa Four Four Two , Vidic: “watu wanasema: ‘Ulikuwa ukipata wakati mgumu sana uliopokutana na Torres’, lakini wanasahau kuwa ilikuwa ni katika mchezo mmoja.
“Nilienda kwa nia ya kutaka kupiga kichea mpira lakini nilibadilisha maamuzi ghafla na kutaka kumpasi Edwin [van der Sar]. Nilikosea mahesabu ya umbali na Torres akafunga.
“Drogba alikuwa ni mgumu. Torres mara nyingi alikuwa akitengeneza nafasi za kufunga, lakini Drogba alikuwa bega kwa bega na wewe muda wote wa mchezo. Drogba alikuwa ana mwili mzito; [Luis] Suarez na [Sergio] Aguero walikuwa bora aisee.”
0 comments:
Post a Comment