Zlatan Ibrahimovic amekanusha tuhuma za zinazolekezwa kwake kuwa ni 'mjivuni'
Msweden huyu (34) alijiunga na Manchester United majira ya kiangazi msimu huu na anatarajiwa kucheza kwa mara ya kwanza nchini England kwenye mchezo dhidi ya Bournemouth.
Amewahi kusema kwamba "Kombe la Dunia bila Zlatan halina ladha kuangalia" na vilevile "Sidhani kama unaweza kufunga magoli hatari kwenye video game".
Lakini Ibrahimovic amesisitiza kwamba yeye ni mtu mwenye misingi imara ya kifamilia na kinachosababisha aongee kauli hizo ni ubora wake na si vinginevyo.
"Mimi ni mtu wa kawaida," alinukuliwa wakati akiongea na Sky Sports.
"Watu wananichukulia mimi kama kijana mbaya; Sijui niko hivi mara niko vile. Watu wanajiuliza: 'Huyu Zlatan yukoje?'
"Mimi ni mtu wa familia. Naijali familia yangu, lakini ninapokuwa uwanjani nabadilika na kuwa Simba. Hii ndiyo tofauti yangu kubwa.
"Siamini kama naringa au najivuna kama watu wanavyodhani. Mimi najiamini. Nina amini kwa kile ninachokifanya. Hiyo haisababishi mimi kuwa na majivuno. Hiko ni kitu ambacho naamini ni kinatokana na uimara binafsi wa mwanadamu.
"Najiamini, na nina imani kwa ninachokifanya. Nina maono na nafanya kila kitu. Najituma kwenye kila kitu.
"Siamini kama nina majivuno."
Video:
0 comments:
Post a Comment