Tuesday, August 16, 2016

Tangu jana kumekuwa na taarifa za kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Mehboob Manji, taarifa ambayo imewashtua Wanayanga wengi sana Dar es Salaam na nchini kwa ujumla.
Taarifa hizo zinadai kwamba nyuma ya sakata hilo kuna wengi wanaohusika akiwemo Mzee Ibrahim Akilimali.
Mzee Akilimali anatajwa kuwa chanzo cha sakata hilo kutokana na hivi karibuni kunukuliwa akihojiwa na moja ya radio nchini akisema uamuzi wa wanachama kuridhia kumkodishia Manji timu ni wa 'kukurupuka' (yaani Manji na wanachama wote wamekurupuka). 
Suala hilo limezua tafrani kubwa kutokana na ukweli kwamba Mzee Akilimali kutokuwa na mamlaka yoyote ya kuzungumzia juu ya masuala ya ndani ya klabu.
Mzee Akilimali alishawahi kutaka kufutwa uanachama wa Yanga baada ya Manji kuitikisha mkutano wa wanachama ili kutoa maamuzi juu ya mzee huyo.
 Ilikuwa ni siku ya mkutano mkuu wa klabu uliofanyika katika ukumbi wa PTA , Jan 19, 2014!Manji aliwauliza wanachama zaidi ya 400 waliokuwepo ukumbini, "Mzee wetu Akilimali anaivunja katiba ya klabu kwa kuongea ovyo kwenye vyombo habari, maneno yake yanaharibu uvunjifu wa utulivu katika timu yetu, Je tumfanyeje mzee wetu?". . Wananchama kwa kauli moja wakajibu "tumfukuze" wakimaanisha avuliwe uanachama. . Kwa busara za Manji akamsamehe,
Hata hivyo leo tena Mzee Akilimali amenukuliwa na moja ya radio akiomba radhi kutokana na kile alichodai ni kutoeleweka vizuri juu ya kauli yake ya 'kukurupuka'.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video