Tuesday, August 9, 2016

Manchester City tayari wametangaza kupata saini ya mlinzi John Stones kutoka Everton kwa ada ya paundi mil 47.5 na kuweka rekodi ya kuwa beki wa pili ghali zaidi duniani.
Stones (22) amesema amefurahi kujiunga na matajiri hao wa jiji la Manchester na kuahidi kupigana kwa nguvu zote kuisaidisa timu hiyo.

“Ninayo furaha kubwa sana kujiunga na Man City na sasa kila kitu kimekamilika na kinachofuata ni kupambana kuhakikisha nasonga mbele zaidi,” aliiambia tovuti rasmi ya Man City.

"Ni dhahiri nimeshuhudia kila kinachoendelea hapa kunako klabu ya Man City, ni klabu yenye malengo ya mbali na yenye kocha bora, hivyo, nasubiri kwa hamu kupata nafasi ya kuitumikia klabu yangu mpya na kufikia malengo.

"Najua haitakuwa rahisi kupata nafasi ya moja kwa moja kwenye kikosi lakini malengo yangu ni kupambana na kuwa moja ya wachezaji wa kutegemewa na kuisaidia mafanikio kwenye timu yangu.

"Nilikuwa na wakati mzuri sana kwenye klabu ya Everton na nawatakiwa kila heri na timu pamoja na mashabiki lakini kwa sasa nitajitolea kwa nguvu zangu zote kuisaidia City."


0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video