Monday, August 8, 2016

Jose Mourinho ameanza kibarua chake Manchester United kwa kutwaa taji la Ngao ya Jamii baada ya Zlatan Ibrahimovic kupachika bao la ushindi dakika za lala salama wakiishinda Leicester City kwenye mchezo uliochezwa jana uwanja wa Wembley, mjini London. 
 Jesse Lingard ambaye alifunga goli katika mchezo wa fainali ya FA Cup dhidi ya Crystal Palace enzi za kocha Louis van Gaal, aliifungia United bao la kuongoza kabla ya mapumziko baada ya kukimbia umbali wa mita 40 na kuwavuka wachezaji wanne na kupasia kamba. 
 Mabingwa wa ligi ya England Leicester City walisawazisha kufuatia makosa  ya Marouane Fellaini kurudisha pasi fupi kwa beki wake na Jamie Vardy akauwahi na kumzunguka David De Gea kisha kufunga goli.
Mshambuliaji 'Mjivuni' Ibrahimovic ambaye amesajiliwa katika kipindi hiki aliifungia bao Man United alipokutana na krosi ya Antonio Valencia na kuiunganisha kwa kichwa na mpira ukamshinda golikipa wa Leicester Kasper Schmeichel.  
Ngao ya Jamii katika namba: 

 21:Idadi ya Ngao za Jamii ambazo Manchester United imewahi kutwaa 
20:Miaka ya Jesse Lingard akiwa mchezaji wa kwanza wa Manchester United kufunga kwenye fainali ya FA Cup pamoja na mchezo wa ngao ya hisani tangu Eric Cantona alipofanya hivyo mwaka 1996. 
97:Hakuna mchezaji mwingine aliyegusa mpira mara nyingi zaidi ya kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater.
 3: washindi wa FA Cup wamefanikiwa pia kushinda Ngao ya Jamii kwenye misimu mitatu iliyopita.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video