Wekundu wa Msimbazi, SIMBA SC, wamelazimishwa sare ya bila kufungana na JKT Ruvu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliopigwa leo (Agosti 27, 2016) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo uliochezeshwa na refa Selemani Kinugani wa Morogoro, aliyesaidiwa na Josephat Bulali wa Tanga na Omar Juma wa Dodoma.
Simba wamefikisha pointi nne baada ya kushinda mabao 3-1 dhidi ya Ndanda FC katika mechi ya kufunguzi wa VPL iliyochezwa Agosti 20 mwaka huu uwanja wa Taifa Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment