IKICHEZA mchezo wa pili kwenye ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu huu, Mbeya City Fc imefanikiwa kuvuna pointi zote tatu muhimu baada ya kuifunga Toto Afican ya Mwanza bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba.
Haruna Shamte lifunga bao hilo mapema dakika ya 7 kwa mpira wa adhabu iliyotplewa baada ya Joseph Mahundi kuangushwa alipokuwa kijaribu kuwatoka waalinzi wa Toto African, hii ilikuwa ni baada ya mashambulizi mfululizo ambayo City iliyafanya kwenye lango la timu hiyo ya Mwanza tangu kipenga cha kuanza mpira kilipopulizwa.
Raphael Daud, Kenny Ally na Joseph Mahundi walicheza vizuri kwenye eneo la kiungo na kuifanya City kung’ara vizuri uwanjani kipindi chote cha kwanza licha ya jitihada za mara kadhaa kutoka kwa wachezaji wa Toto jambo lililohitimisha dakika 45 za kwanza ubao ukisoma 1-0.
Kipindi cha pili,kocha Kinnah Phiri aliwatoa Salvatory Nkulula na Geoffrey Mlawa aliyeumia na nafasi zao kuchukuliwa Ditram Nchimbi na Michael Kerenge mabadiliko ambayo yaliongeza nguvu ya mashambulizi kwa City lakini kupungua kwa umakini kwenye eneo la mwisho kulihitimisha dakika 90 bao likisalia hilo 1-0.
Mara baada mchezo huo, Kocha Phiri amewapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizuri, na kuwataaka kujituza na kuwa tayari kwa mchezo mwingine mwishoni mwa juma lijalo.
0 comments:
Post a Comment