Haikuwa ngumu kugundua kwamba haya ni mazoezi ya kwanza kwa John Stones katika klabu ya Manchester City.
Mlinzi huyo wa England alionekana kama mtoto mdogo ambaye amehamishwa shule, alijawa na upweke.
Wakati wachezaji wenzake wanaingia kwa makundi kwenye uwanja wa mazoezi, Stones alikuwa mnyonge nyuma ya Sergio Aguero.
Straika huyo wa Argentina alionekana kutovutiwa kuzungumza na Stones.
Wakiwa uwanjani, wachezaji walikuwa na furaha huku wakitaniana, lakini Stones hakuwa sehemu yao. Huenda itamchukua wiki kadhaa mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa paundi milioni 47.5 kujichanganya na wenzake.
Dhahiri wiki chache zijazo ataingia kwenye utani na wenzake pamoja na kushikana mikono kama ilivyo kwa wanandinga wenzie chini ya kocha Pep Guardiola.
0 comments:
Post a Comment