Manchester City Licha ya kushinda 3-1 dhidi ya West Ham United, Mechi imezua utata kwa tukio la Kipindi cha Pili la Straika wa City, Sergio Aguero, kumpiga kiwiko Beki wa West Ham Winston Reid bila Refa Andre Marriner kuona na sasa ipo hatari FA, Chama cha Soka England kumchukulia Mchezaji huyo hatua na kumfungia.
Chama cha soka cha England, FA, kinatarajia kutoa maamuzi yake kutokana na tuko hilo na ikiwa Aguero atafungiwa mechi tatu basi ataikosa Dabi ya Manchester huko Old Trafford Septemba 10 kwenye Mechi ya EPL pamoja na ile dhidi ya Bournemouth na mechi ya Raundi ya 3 ya EFL CUP na Swansea City.
0 comments:
Post a Comment