Kikosi cha
vijana wenye umri chini ya miaka 12 cha klabu ya Barcelona mwishoni mwa Juma lililopita
kilitwaa Ubingwa wa mashindano ya vijana nchini Japan kwa kuwachapa bao 1-0
wenyeji Omiya Ardija Junior, lakini kinachogonga vichwa vya habari kwasasa sio
matokeo ya mechi hiyo.
Kupitia
mtandao wao wa Twita, Barcelona wame-post video yenye maneno yanayosomeka
FairPlay yaani mchezo wa kiungwana ambayo inawaonesha vijana wake wakiwafaraji vijana
wenzao wa Omiya baada ya kuwaburuza na kupoteza kombe wakiwa kwenye ardhi yao.
Baada ya
kuwachapa Wajapan hao, nyota hao wa miamba ya soka la Hispania, Barca, walimtia
moyo kila mchezaji wa timu pinzani ambapo wengi wao walikuwa wakimwaga machozi.
Tendo hilo
la upole liliongozwa na Nahodha wa Barcelona Adria Capdevila Puigmal – na sasa
limewagusa mashabiki wa kandanda Duniani kote.
Barcelona walioshinda mabao manne kwa bila
dhidi ya Ventforet Kofu mechi ya ufunguzi, halafu nusu fainali wakachomoza na ushindi kama huo mbele ya Tokyo
Verdy Junior , walijikuta wakipata wakati mgumu zaidi kwenye mechi ya fainali
ambapo walishinda kwa mbinde goli moja kwa Nunge na baada ya kipyenga cha
mwisho waliwapongeza wapinzani wao kwa kiwango kikubwa walichoonesha.
Kitendo hiki
kilikumbushia namna nahodha wa zamani wa Barcelona, Xavi alivyomfariji
Andrea Pirlo baada ya Barca kushinda mabao matatu kwa moja katika fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya mwezi Juni 2015 mjini
Berlin, Ujerumani.
0 comments:
Post a Comment