Wednesday, August 17, 2016

Utata wa kwamba mchezaji Hassan Kessy atacheza au hatocheza mechi ya Ngao ya Jamii kati ya klabu yake mpya ya Yanga dhidi ya Azam FC mechi inayotarajiwa kuchezwa Jumatano August 17 umepetiwa ufumbuzi na hatimaye beki huyo wa zamani wa Simba SC ameruhusiwa kucheza mechi hiyo.
Habari za uhakika zilizoripotiwa na Tovuti ya michezo ya shaffihdauda.co.tz zinadai kwamba, hatua hiyo imefikiwa baada ya kikao cha kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kushindwa kufanyika na badala yake kitafanyika Alhamisi huku mechi ya Ngao ya Jamii ikitarajiwa kupigwa Alhamisi siku moja kabla ya kikao kufanyika ambacho kitatoa majibu ya kesi mbalimbali zinazohusu usajili.
“Leo kulikuwa kunatakiwa kukaa kikao cha kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kwa ajili ya kupitia kesi zote za usajili ikiwemo ya Kessy. Lakini kikao hicho hakikufanikiwa kufanyika na badala yake kitafanyika Alhamisi,” amesema Jonas Kiwia Kaimu Mkurugenzi wa mashindano wa TFF.
Kwahiyo wameamua kwamba, wachezaji wote ambao waliombewa leseni na klabu zao, wataruhusiwa kucheza mechi ya kesho. Kwa maana hiyo, Hassan Kessy Ramadhani anaruhusiwa kucheza mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video