Thursday, August 11, 2016

URA FC ya Uganda inatarajia kucheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya Azam FC na Simba SC ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya soka ya Uganda.
Mechi ya kwanza ni kesho Ijumaa ambapo Wakusanya Mapato hao wa Uganda watapambana na Azam FC uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuanzia majira ya saa 10:00 Jioni na itakuwa live kupitia AZAM TWO.
Simba nao watacheza na URA Jumapili na URA uwanja wa Taifa Dar es salaam na mtanange huo pia utakuwa Live AZAM TWO.
Kocha mkuu wa timu hiyo, Kisala Kefa , ameiambia Tovuti rasmi ya URA kuwa: " Nina furaha kupata mechi mbili za kirafiki za kimataifa, naamini nitawapima wachezaji na itatusaidia kuelekea msimu mpya wa 2016-2017 wa ligi kuu ya  Azam Uganda Premier league”.
Mfarasa wa wachezaji 25 ukijumuisha na viongozi wa klabu akiwemo Mkurugenzi wa Ufundi Kyondo Geoffrey utatua leo jijini Dar es salaam kwa ndege.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video