Wednesday, August 17, 2016

Zikisalia saa chache kabla ya Yanga SC kuivaa Azam FC katika mechi ya Ngao ya Jamii inayochezwa leo saa 10:00 Jioni Uwanja wa Taifa, Dar es salaam, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga ambaye kwasasa amefungiwa mwaka mmoja kutojihusisha na soka, Jerry Muro,  ame-post picha Instagram yenye ujumbe unaoashiria Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, ameamua kuendelea na wadhifa wake.
Taarifa hiyo inakuja baada ya jana Viongozi wa Matawi ya Wanachama wa Yanga Jijini Dar es salaam kukutana kwa dharura makao makuu ya klabu yao, Jangwani, wakipinga na kukanusha taarifa za Manji kudaiwa kujiuzulu nafasi yake kwa madai kuwa amechoka kusakamwa na kutukanwa na baadhi ya wanachama wa Yanga.
Hata hivyo, taarifa za ndani zilieleza kuwa ni kweli Manji alidhamiria kuachana na Yanga, lakini baada ya juhudi kubwa kufanyika wakimsihi asifanye hivyo, Jerry Muro amethibitisha kwamba Manji amrejea kama kawaida. (Tazama picha hapo chini).
Mtafaruku huu unakuja siku chache tangu Manji atangaze nia yake ya kutaka kuikodi Yanga kwa miaka 10 ikiimiliki nembo na klabu yenyewe, jambo ambalo liliridhiwa na Wanachama wa Yanga kwenye mkutano mkuu wa Agosti 6 mwaka huu Ukumbi wa Diamond Jubilee.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video