Mashindano ya Olimpiki ya Rio 2016 yanazidi kushika kasi mjini Rio de Janeiro, Brazil ambapo Mataifa mbalimbali yanaendelea kuzoa medali.
Taifa lenye wanamichezo wengi zaidi, Marekani, linaongoza kwa kujikusanyia Jumla ya medali 50 mpaka sasa ambazo zinatokana na medali 20 za dhahabu, 13 za fedha na 17 za Shaba.
China nayo imekomaa katika nafasi ya pili kwa kuzoa medali 13 za dhahabu, 10 za Fedha na 14 za shaba, Jumla ni medali 37.
Nafasi ya tatu wapo Uingereza waliofanikiwa kijiwekea kibindoni Jumla ya medali 22 ambazo ni 7 za dhahabu, 9 za Fedha na 6 za Shaba.
0 comments:
Post a Comment