Tuesday, August 16, 2016

Baada ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC kukutana jana na Mfanyabiashara Maarufu na Mwanachama wa klabu hiyo, Mohamed Dewji 'MO' kujadili  mabadiliko ya uendeshaji wa timu hiyo kutoka Wanachama wa kawaida kwenda mfumo wa Hisa ambao ni wa kisasa, hamu ya wanachama na wapenzi wa Simba ni kujua kilichojiri katika kikao hicho maalum.
Majadiliano hayo yanayoaminika kuwa na matunda mazuri yalifanyika Hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Hajji Sunday Manara amethibitisha kwamba kikao kilikwenda vizuri na mambo mazuri yanakuja.
Manara ameeleza kwamba Wanasimba watulie na kesho (Jumatano) atakuwa na mkutano na Waandishi wa Habari ambapo atatoa ripoti rasmi ya majadiliano hayo kwa Umma wa Tanzania.
MO anahitaji kupewa asilimia 51 za hisa kwa dau la Bilioni 20.
MPENJA SPORTS itakuletea habari zote kuhusu suala hilo..endelea kuwa nasi...

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video