"Ruvu Shooting Vs Stand United, ni mchezo wa kirafiki wa kihistoria utakaochezwa uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Kibaha, Pwani leo Jumamosi August 13, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni.
Msimu wa mwaka 2014/15 Ruvu Shooting ilishushwa Daraja na Stand United katika uwanja wa Kambarage, Shinyanga kwa kufungwa bao 1-0.
Tangu kipindi hicho, timu hizi hazikuwahi kukutana na kucheza mchezo wowote wa kirafiki au mashindano.
Nani ataibuka nani katika mchezo huo? Njoo Mabatini leo ushuhudie mwenyewe". Taarifa ya Masau Bwire, Afisa habari wa Ruvu Shooting.
0 comments:
Post a Comment