Saturday, August 6, 2016

Paul Pogba hajasaini kunako klabu ya Manchester United huku suala lake bado likiendelea kugonga vichwa vya habari vya vyombo mbalimbali. Inaonekana dhahiri shahiri Mfaransa huyo ana uhitaji mkubwa sana wa kurudi kwenye klabu yake hiyo ya zamani chini ya bosi mpya.

Uhamisho wa aina kama hii si mara ya kwanza kutokea kwenye medani za soka, na ndio maana United wanaonekana kuwa watulivu kabisa. Lakini wasingefanya hivyo kama ingekuwa dirisha linaelekea ukingoni. Bado kuna pande tofauti ambazo zinaokana kuwa bado hazijafikia makubaliano. Zama hizi zimebadilika, sio zile zama za kusaini tu mkataba na kuanza kucheza soka, kuna mambo mengi sana, kuna ishu ya masuala ya masoko pamoja na hakimiliki ya matangazo kati ya klabu na mchezaji.

Kwa wiki kadha sasa, United wameonekana kufikia karibu kabisa kuinasa saini ya kiungo huyo, lakini kwasababu mambo bado hayajawa rasmi, mashabiki wameanza kuingiwa na mshangao kwamba nini hasa kinaendelea pamoja na vyombo mbalimbali vya habari.

Kwa mashabiki wa United, mikakati ya usajili huu wa Pogba ndiyo imetawala kama ule uliotokea kwa Alan Shearer mwaka 1996 na Wesley Sneijder mwaka 2011. Kati ya wachezaji hao, hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kusajiliwa na United. Shearer aliamua kujiunga na klabu ya nyumbani kwao Newcastle ambao walilipa fedha iliyovunja rekodi wakati huo paundi mil 15, vile vile kwa Sneijder ambaye alibakia Inter Milan.

United hawakushawishika kwamba wawili hao wote wasingeweza kuja klabuni hapo. Kwa pogba wanaamini kwamba ni rahisi kuja kwasababu ya ukubwa wa klabu vile vile ni kijana ambaye walimlea wenyewe.

Mwanzoni kabisa mwa mwaka huu, uhamisho wake ulianza kugonga sana vichwa vya habari vya vyombo mbalimbali, hata kama wachezaji wenzake wa Juve walifurahi kumwona akibaki jijini Turin na kuwafanya wawe na nguvu ya kupigania taji la Uefa ipasavyo.

Kulikuwa na vilabu vingi vilizotajwa katika uhamisho wake, vilabu hivyo ni pamoja na Real Madrid, Barcelona, Manchester City na United wenyewe


Kwa upande wa Barca ni wazi kwamba kiasi hiki cha fedha wasingeweza kukimudu kwasababu wako kwenye mchakato wa kujijenga upya kiuchumi. Madrid walikuwa na nia ya kweli kabisa na walikuwa na nafasi kubwa pia kwa kuwa walikuwa ni mabingwa wa Uefa na vile vile kocha wa timu hiyo Zinedine Zidane anatoka taifa moja na Pogba. Lakini wameonekana kuishia njiani kwenye dili hili.

Mtendaji Mkuu Msaidizi wa Man United Ed Woodward miaka mitatu iliyopita alisema kwamba wasingeruhusu klabu yoyote kuwapiku kwenye usajili wa mchezaji huyo, na sasa ni yeye huyo huyo ambaye amelifanyia kazi suala la usajili huu wa Pogba, mchakato ambao ulihusisha kukutana na mchezaji huyo na wakala wake huko Florida mwezi uliopita.

Pengine pesa inawezekana sio kitu kikubwa sana, ila mtazamo ungekuwa kwamba kuna sehemu nzuri zaidi za kuishi kuliko jiji la Manchester, au pengine kuna unafuu wa kodi kwenye nchin nyingine zaidi ya England, au kuna timu nyingine bora zaidi ya United ambao walimaliza nafasi ya tano kwenye msimamo wa EPL. Kurudi kwenye klabu yake ya zamani halikuwa chaguo la kwanza kwa Pogba mwoshono kabisa mwa msimu uliopita.

Baada ya kuona hivyo United waliamua kupandika mawazo chanya kwa mchezaji, walisisitiza sana juu ya utajiri wa klabu kwa wawakilishi wa mchezaji huyo. Vile vile walimpandikiza sumu kwamba kama angeenda Madrid, basi angekuwa mchezaji wa nne kwa thamani nyuma ya Cristiano Ronaldo, Gareth Bale na Benzema.

Wakasema kama Pogba angejiunga na United wao wangemfanya kuwa namba moja, timu ingejengwa kumzunguka yeye na thamani yake ingezidi kuwa kubwa zaidi duniani. Hayo yote yaliwafurahisha Adidas, ambao walisaini naye mkataba wa euro mil 40 mwezi March baada ya kuwachagua wao badala ya Nike kwaajili ya kuwatangazia bidhaa zao. Na uzuri ni kwamba United nao wanavaa Adidas.

Sasa kutokana na yote hayo, imekuwa ni rahisi zaidi kwa wakala na wawakilishi wengine wa mchezaji huyo kukubali ofa ya United kutokana na viashiria vyote vilivyooneshwa na United ikiwemo dau nono.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video